Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amekutana na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kufahamiana na kujadili mambo kadha wa kadha ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Shinyanga.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho,Telack alisema huu ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/2017 – 2020/2021 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya maendeleo ya watu.

“Ili kutimiza malengo ya mpango huu lazima serikali ifanye kazi kwa ushirikiano wa karibu na sekta binafsi na nyinyi ni sehemu ya sekta binafsi na ili kudumisha ushirikiano huo serikali imeanzisha mabaraza ya biashara katika ngazi ya taifa,mikoa na wilaya”,alieleza Telack.

Aidha alisema uwekezaji ni moja ya shughuli zinazochochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla ambapo hadi sasa mkoa huo una jumla ya viwanda 81,ambapo viwanda vikubwa ni 18,viwanda vya kati 9 na vidogo 54.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa kikao chake pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 20,2017.
Wafanyabiashara,wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa ukumbini 
Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy akizungumza katika kikao hicho. 
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akichangia hoja katika kikao hicho .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...