Serikali ipo katika hatua za mwisho katika kuhidhinisha bilioni 1.6 kutoka katika mfuko wa hifadhi za jamii GEPF kwaajili ya kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC).

Akizungumza jana katika kiwanda hicho mara baada ya kutembelea Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho kwa lengo la kufufua kwa kuwa kiwanda hicho kinabeba dhana nzima ya maendeleo ya uchumi wa viwanda kwenye nchi ya Tanzania

Alisema kuwa mfuko wa GEPF baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Rais akihimiza Serikali ya viwanda ,wameweza kujiridhisha kuwa wanauwezo wa kuwekeza katika kiwanda hicho cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC)

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,wa pili kulia jana alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira na wa kwanza kulia ni Meneja mkuu Kilimanjaro Machine Tools Eng.Adriano  Nyaluke akitoa taarifa za uzalishaji wa kiwanda hicho(Picha na Pamela Mollel Arusha).
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama akiteta jambo na wakurugenzi wa mifuko ya jamii jana katika ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangi ,kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF Mh. William Erio.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiwa anatoa maelekezo katika kiwanda hicho ambapo alisema kuboreshwa kwa kiwanda hicho kitasaidia ajira kwa vijana
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiangalia baadhi ya vyuma vilivyo zalishwa katika kiwanda hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi kisheria hela iliyoko katika Mifuko ya Mafao ya Kustaafu au Retirement Benefits Funds Ni Mali ya Mwajiri au Mwajiriwa!? Je, kusudi Fedha iwekezwe je Serikali ambayo Kimsingi Ni Mwajiri anayo mamlaka juu ya hela hiyo !? Nadhani, suala hili lnahitaji utafiti kwani itafika mahala mstaafu anakuta hawezi kupata Mafao kutokana na uwekezaji usiofanyiwa upembuzi WA kina WA faida na hasara ya matumizi ya fedha! Ni jambo muhimu hasa SSRA km ina nguvu kusimamia jinsia hela inavyowekezwa vingine wastaafu watapata shida sana huko mbele na pengine kufa bila Mafao na hivyo, Mifuko kufaidika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...