Serikali imemuagiza Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kuwasiliana na Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) ili kupata gari la Zimamoto ili ndege za Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ziweze kuanzisha safari zake katika Mkoa wa Katavi.

Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema kwa muda sasa kiwanja hicho kimekuwa kikitumiwa na ndege chache za Shirika la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), hivyo ni wakati sasa kutumika na ndege zetu ili kuboresha huduma za usafiri wa anga Mkoani hapa.

“Kamilisheni mazungumzo na KADCO ili kupata gari la Zimamoto lenye ujazo wa Lita 4,000 litakalokuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya moto endapo yatatokea, kutakapokuwa na gari hilo uwanjani hapa tutaanzisha safari za ndege za Shirika letu wakati ndege yetu ta tatu itakapowasili,” amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, amemtaka meneja wa Uwanja huo wa ndege kuhakikisha anaingiza uwanja huo katika mpango maalum kwa ajili ya ujenzi wa taa kiwanjani hapo ili uwanja huo uweze kutumika kwa mchana na usiku.

Eng. Ngonyani ameongeza kuwa azima ya Serikali ni kuhakikisha usafiri wa anga nchini unaimarika kwa kutumia ATCL na mashirika mengine yalipo nchini hivyo kama Serikali imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja ili viwe katika viwango vinavyokubalika.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Mpanda Seth Lyatuu (kushoto) wakati alipokagua huduma za uwanja huo Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani(Kulia) akikagua Mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielekroniki katika Stesheni ya Mpanda Mkoani Katavi. Katikati ni Meneja Mradi wa kampuni ya Makgroup Ltd Bw. Joseph Mrosso.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Reli Tanzania, Kanda ya Tabora Bw. Frederick Masangwa(Katikati), wakati alipokagua huduma za usafiri wa Reli Mkoani Katavi.
Meneja wa Msimamizi wa Bandari ya Kigoma Bw. Morris Mchindiuza (aliyenyoosha mkono) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) eneo itakapojengwa bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili) akitoka kukagua kingo za bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...