Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuwajali na kuwahudumia wagonjwa kwa kupeleka idadi ya waganga, wauguzi, dawa na utoaji wa vifaa tiba katika zahanati vituo vya afya na hospitali za wilaya nchini .

Pia Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha katika kila Kata na Wilaya kunajengwa zahanati na vituo vya afya ili kunusuru pia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano .

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipotembelea katika kituo cha Afya cha kijiji cha Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma katika siku ya pili ya ziara yake kuona utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm katika maendeleo ya kisekta.
Shaka alisema serikali ya Chama Cha Mapinduzi zina wajibu wa kufuatilia kwa karibu na kujua kama yale yote yalioahidiwa katika ilani , yanayotimizwa na iwapo yanawafikia na kuwahudumia wananchi kama inavyokusudiwa na serikali Kuu kwa wananchi wake. 

Alisema pamoja na kukabiliwa na upungufu wa idadi ya Waganga na Wauguzi katika Kituo cha Afya Nguruka, waliopo wamekuwa wakijituma bila kuchoka huku wakitoa huduma kwa njia makini na sahihi ili kunusuru na kutibu wagonjwa . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...