THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SHONZA AMWAGA MINOTI, SONGWE

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (CCM) ametimiza kwa vitendo   ahadi yake ya kuwawezesha kiuchumi wanawake ambao ni wafuasi wa CCM kwa  kukusanya zaidi ya Sh35 milioni  ambazo wanawake hao walioko kwenye vikundi vya ujasiriamali wapatiwa mtaji wa kiasi cha Sh320,000 kwa kila kikundi.
Kati ya fedha hizo, Sh 20 milioni zilitolewa na Shonza huku wadau wanaomuunga mkono mbunge huyo wakitoa zaidi ya Sh15 milioni katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM kiuchimi ambao ulizinduliwa rasmi juzi na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson.
Akizungumzia mradi wa uanzishwaji wa mfuko huo, Shonza alisema  moja ya ahadi zake wakati wa kampeni za kuomba ridha ya kuchaguliwa na wanawake mwaka 2015, aliwahakikishia kuwainua kiuchumi na baada ya kuchaguliwa alianza na utaratibu wa kukutana wanawake kwa kila kata  kwa ajili ya kuunda vikundi, kuvisajili ili viweze kukopesheka.

Alisema jambo lililofanywa na Shonza ni mfano tosha na kudhihiridha kwamba anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya CCM n azma ya Serikali ya kufikia  nchi ya viwanda.
Katika uzinduzi, huo, Mbunge Shonza  aliungwa mkono na wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Jimbo la Mtama, Livingstone Lusinde ‘Kibajaji’, Mbunge wa Jimbo la Pangani Tanga, Jumaa Awesu, Janeth Mbene wa Ileje na Josephat Hasunga wa wa Jimbo la Vwawa Mbozi.
“Tayari kuna kikundi kwa kila kila kata ambavyo nilivisimamia mimi kuanzia kupta usajili na vingine vimeanza kazi za ujasiriamali na vina vifanya kazi, kwa kila kikundi niliahidi kuwasaidia Sh200, 000 kama mtaji wa kuanzisha shughuli yoyote ya ujuasiamali, lakini nikaone niwakutanishe wadau wengine watakaoniunga mkono kwenye hili na nashukuru mmeonesha ukweli wenu”.
Alisema wanawake wa Songwe hawahitaji kutafutiwa kazi maofini, kwani  ni wachapa kazi lakini changamoto waliyo nayo ni mitaji tu kwani uwezo wa kuingia shamba na kuanzisha mradi wowote wa kiujasiriamali wanao.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Tulia aliwataka wabunge wa viti maalum nchini kwenda kutekeleza ahadi walizozitoa  kwa wananchi wakati wakipigiwa kura badala ya kuwatelekeza kwa kisingizio cha kutokuwa na majimbo.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (katikati) wakiwa wamekumbatia kitita cha fedha kiasi cha Sh35 milioni zilizotolewa katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali katika vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320, 000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe. 

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza wakipanga vizuri kitita cha fedha kiasi cha Sh35 milioni zilizotolewa katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali kupitia vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320,000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe. 
Wabunge wakicheza muziki na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Songwe, waliofika kwenye harambee ya uzinduzi wa harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali katika vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320, 000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe.