Marehemu Mzee Matthew Gordon Kayuza

Familia ya Marehemu Mzee Matthew Gordon  Kayuza ya Ada Estate Kinondoni Dar Es Salaam inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa niaba ya koo za Kayuza, Daudi Kolawa, Samatta, Mbiza, Poyo, Sentimea, Chienela na Nshunju kwa kuwafariji kwa hali na mali kipindi chote cha kumuuguza na hatimaye kifo na mazishi ya baba yao mpenzi Mzee Matthew Gordon Kayuza aliyefariki tarehe 21/06/2017 katika hospitali ya Aga Khan na kuzikwa tarehe 24/06/2017 kwenye makaburi ya Kinondoni Dar Es Salaam

Shukrani za pekee ziwafikie wafuatao: Waheshimiwa Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamisi Juma, Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, na Mama Salma Kikwete. Uongozi na wafanyakazi wa NSSF, Indian School, Dar Es Salaam, na Bank M, Madaktari na manesi wa Aga Khan Hospitali DSM, Dr. Jerusalem Makotore, Dr Gabriel Ndunga na manesi Esther, Joyce na Neema ambao walikuwa wakimhudumia Mzee nyumbani, Wachungaji, wahudumu na kwaya ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano,Rev.Canon Albano Mbulinyingi, Jumuiya ya Mtakatifu Theresia ya Kanisa la Kristo Mfalme Kinondoni, majirani, ndugu na marafiki.  

Kutakuwa na mkesha wa kumaliza msiba leo Ijumaa tarehe 28/07/2017 kuamkia Jumamosi tarehe 29/07/2017 nyumbani kwa Marehemu Ada Estate, Kinondoni. Itafuatiwa na ibada ya shukrani siku hiyo hiyo ya Jumamosi saa mbili  asubuhi katika Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano Posta Dar Es Salaam. Nyote mnakaribishwa.

“BABA MZEE MATTHEW KAYUZA TULIKUPENDA SANA ILA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI, PUMZIKA KWA AMANI, DAIMA UTAENDELEA KUISHI NDANI YA MIOYO YETU”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...