THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SIMBA KUELEKEA SAUZI KWA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI

Timu ya Soka ya klabu ya Simba kesho alfajiri, inatarajia kwenda nchini Afrika kusini, kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. 

Kambi hiyo ya siku Ishirini itahusisha wachezaji wote waliosajiliwa kwenye klabu,kwa msimu huu wa ligi. 

Kwa upande wa wachezaji waliopo kwenye Timu ya Taifa,wao wataungana na wenzao,mara baada ya mchezo wa marudiano baina Taifa Stars na Rwanda,utakaochezwa wiki ijayo kule Kigali. 

Ikiwa huko nchini Afrika kusini, kikosi hicho pia kitapata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu,kabla ya mchezo wake wa tarehe nane mwezi ujao(SIMBA DAY),Mechi ambayo klabu huitumia kutambulisha wachezaji wake na jezi mpya ya msimu,mchezo huo utapigwa hapa jijini Dar es salaam,kwenye uwanja wa Taifa. 

Wakati huo huo klabu ya Simba inaungana na wanamichezo na watanzania wengine,kumpa pole Waziri wetu mwenye dhamana ya michezo nchini Dr Harrison Mwakyembe kwa kuondokewa na Mkewe bi Linnah Mwakyembe. 

Tunamuomba Waziri Mwakyembe awe na subira yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu,na klabu itashiriki shughuli zote za msiba wa mama yetu Linnah. 

IMETOLEWA NA 
IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO 
SIMBA NGUVU MOJA