THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SIMULIZI: KITANDA CHA SOKWE MTU na Dokta Mungwa Kabili


Ni simulizi la ukweli linalo husu maisha ya kijana Lugwisha kutoka kitongoji cha Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora ambaye baada ya kumaliza shule ya msingi mnamo mwaka 1994 huko kijijini kwao, alifunga safari hadi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutafuta maisha. 


 Miaka kumi baadae kijana Lugwisha akawa amepata mafanikio makubwa yaliyobadilisha maisha yake. Mafanikio katika maisha ya Lugwisha yanasababisha kuinuka kwa maadui ambao hawapendezwi na kufanikiwa kwake. Maadui hawa wanapanga njama mbalimbali za kupambana dhidi ya mafanikio ya Lugwisha. 

Kati ya maadui wa Lugwisha, ni maadui wawili tu ndio wanaonekana kuwa na nia thabiti na ya dhati katika mapambano dhidi ya Lugwisha. Maadui hao ni Beka Msangi pamoja na Bundala. 
Beka Msangi alikuwa mmiliki wa bar iliyo kuwa jirani na bar iliyo milikiwa na Lugwisha. Bar hii ya Lugwisha ilikuwa ni moja kati ya makumi ya vitega uchumi vyake vilivyo muingizia fedha nyingi. Bar ya Lugwisha ilikuwa maarufu sana jijini Dar es Salaam na ilikuwa ikifurika wateja kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. 
Bar hii ya Lugwisha ilikuwa katika eneo lenye bar nyingi. Uwepo wa bar ya Lugwisha katika eneo hilo uliua biashara ya karibu bar zote zilizo kuwepo katika eneo ikiwemo bar ya Beka Msangi. Beka Msangi hakutaka kukubaliana na hali hiyo na hivyo kufikia uamuzi wa kusafiri hadi katika kijiji cha Mchukwi wilayani Rufiji mkoani Pwani, kwa ajili ya kumroga Lugwisha. Baada ya kupiga ramli, wachawi wa Rufiji wanaona njia pekee ya kupambana na Lugwisha ni kumuhamisha kichawi yeye na bar yake kwa kutumia uchawi wa Kizigua, ujulikanao kama “Sunkwa”.