THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SPIKA WA BUNGE APOKEA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SEMENTI NA HUNDI YA SH. MILIONI 15 KUTOKA BENKI YA CRDB TAWI LA DODOMA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU, WILAYANI KOGWA, DODOMA.Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akipokea hudi ya shilingi milioni 15 na msaada wa Mifuko mia mbili (200) ya sementi kutoka kwa Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) waliotoa ili kusaidia ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kogwa, Dodoma. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akionyesha hudi ya shilingi milioni 15 aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Msafiri Simon.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hudi ya shilingi milioni 15 na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya sekondari Laikala, Kogwa, Dodoma. Walioshikilia hundi hiyo ni Wanafunzi wa shule hiyo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Walimu, Wanafunzi wa shule ya Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma na wakazi Kata ya Saranga (hawapo pichani), mara baada ya kupokea msaada huo kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia Diwani wa kata ya Sagara Ndg. Simon Kamando.

(Picha na Ofisi ya Bunge)