Nahodha msaidizi wa timu ya New York, Elisante Shayo akikabidhiwa uzi na Malkia wa Nyuki wa timu ya New York tayari kwa mchezo wao wa Jumamosi hii dhidi ya D.C. 
Timu ya New York Tanzania Community a.k.a NYATI  wapo tayari kwa mchezo wao dhidi ya timu ya Watanzania kutoka Washington D.C Jumamosi hii ya Julai 15, 2017  kuanzia saa nane mchana katika viunga vya Lincoln Park, Nj.
Mchezo huu ni wa kukata na Mundu na siyo wa kukosa maana historia ya machungu ya timu New york siyo ya kubeza kutokana na kupokea kipigo cha nusu dozen miaka miwili iliyopita vijana wamesema labda itokee tu safari hii D.C watatafutana na kama siyo kutafuta njia ya kutokea uwanjani baada ya  kupata kipigo na vijana wa New York watakae ongozwa na vijana wenye damu mchanganyiko kutoka vyuo  vya mafunzo.  
Vijana wamejitolea kuwafuta machozi wapenzi wao watakaokuwa wakiwachagiza  kwenye uwanja wanyumbani siku hiyo. Kabla ya Mchezo mwamuzi ataanza kukagua (Identity Card ) ya kila mchezaji ilikuondowa utata wa kupata watalii wasiokuwa na tija ya kizalendo, kwani Uzalendo wa Kitanzania kwanza.
Address ni hii: 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...