THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

TAARIFA KWA WAPENZI NA WASHABIKI WA FM ACADEMIA BAND

Wamiliki wa bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” wametoa ufafanuzi juu ya kile kilichopelekea Nyoshi el Saadat kuvuliwa cheo cha urais wa bendi.

Wiki mbili zilizopita Nyoshi alivuliwa cheo hicho alichokitumikia kwa takriban miaka 20 na nafasi yeke kuchukuliwa na Patcho Mwamba, hatua ambayo imezua fikra tofauti miongoni mwa mashabiki wa muziki wa dansi – wengine wakiona Nyoshi kaonewa na wengine wakiunga mkono mabadiliko.

Blake Mwambona ambaye amejitambulisha kama mdogo wa aliyekuwa mmiliki wa FM Academia (Marehemu Martin Kasyanju), amesema kwamba kwa zaidi miezi sita iliyopita, maendeleo ya bendi yamekuwa yakididimia kwa kasi kuwa, ikiwa ni pamoja kukosekana ari kwa wanamuziki wengi.

Mwambona amesema wanaamini mfumo wa kubadilishana uongozi, ndio bora zaidi badala kumsimika mtu uongozi kwa miaka mingi na mwisho wa siku anageuka kuwa mtawala. 

Naye Nsajigwa Martin Kasyanju ambaye ni mtoto wa marehemu Martin Kasyanju, amesema kuwa wao hawajamfukuza Nyoshi, ila akiamua kuondoka hawana kizuizi.Tayari imedaiwa kuwa Nyoshi yuko chimbo akisuka bendi yake mpya na hajakanyaga show za FM tangu avuliwe urais wa bendi.

Katika mahojiano yake na Jembe FM ya Mwanza wiki mbili ziliyopita, Nyoshi alifunguka kuwa ameachana na FM Academia na ataibuka na bendi mpya. 

“Hatujamfukuza, tumebadili uongozi wa bendi kwa manufaa ya biashara yetu, kama yeye hawezi kuishi FM bila cheo cha urais, hatutakuwa na namna ya kumsaidia. Kwetu sisi biashara kwanza halafu mambo mengine baadae", Japo yanasemwa mengi, hata hivyo sisi tunatambua Nyoshi bado ni muajiliwa wa FM Academia kama mikataba inavyojieleza na taratibu za kazi zilivyo, anaeleza Nsajigwa.

“Tunathamini sana mchango wa Nyoshi, lakini ni lazima ifahamike kuwa FM Academia inafanya biashara, kuna wakati maamuzi magumu lazima yachukuliwe kwaajili kulinda biashara” aliongeza Nsajigwa na kufichua kuwa mabadiliko hayo yameongeza furaha, amani na ari kwa wanamuziki wa FM Academia.