THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Taasisi ya MO Dewji yatunukiwa tuzo ya ubora ya Superbrand

Taasisi ya MO Dewji Foundation inayojuhusisha na kusaidia jamii katika elimu, afya na maendeleo ya jamii imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora inayofahamika kama SuperBrand. Taasisi hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji imetunukiwa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ambayo inaifanya. 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema ni heshima kubwa kwa taasisi kupata tuzo hiyo lakini pia itawasaidia kufanikisha miradi mikubwa ambayo wamepanga kuifanya na taasisi kubwa kama ya Bill Gates.

“Kwa niaba ya Taasisi ya MO Dewji na kampuni ya MeTL Group tunashukuru sana kwa tuzo hii na huu ni mwanzo mpya wa safari yetu, kama mnavyojua taasisi yetu ilianzishwa mwaka 2014 na katika kipindi cha miaka miwili tumeanzisha miradi mbalimbali kama MO Entrepreneurs na MO Scholars ikiwa na lengo la kuwasaida vijana na tunafuraha Baraza la SuperBrands limetutambua.


“Tuzo hii inatusaidia katika miradi mikubwa kwa sasa kama taasisi ya Mohammed Dewji tunataka kufanya ushirikiano na taasisi kubwa kama Taasisi ya Bill Gates, kushirikiana na taasisi za Kenya, Uganda, UK, jina la Mohammed Dewji litakuwa la kwanza na SuperBrand litakuwa ya pili,” amesema Barbara. .
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez tuzo ya ubora ya SuperBrand.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya ubora ya SuperBrand.


Tuzo ya SuperBrand ambayo Taasisi ya MO Dewji imetunukiwa.