TAHMEF (Tanzania Health and Medical Education Foundation) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO), lililozinduliwa rasmi tarehe 8 Julai 2016 na Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee Mhe Dr. Hamisi Kigwangalla.

Tarehe 8 Julai 2017 TAHMEF ilitimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, na katika maadhimisho hayo TAHMEF imetoa huduma bure ya upimaji wa Saratani ya shingo ya kizazi, wilayani Kondoa, mkoani Dodoma katika viwanja vya hospitali ya Wilaya.

Zoezi hilo liliendeshwa kwa Muda wa siku mbili (8-9 julai 2017) zaidi ya wanawake 500 Wilayani kondoa walijiandikisha na kupata huduma bure ya elimu na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.

Hivi sasa TAHMEF inaendesha mradi uitwao NURU YA AFYA unaolenga kuwezesha wanawake wasio na ajira rasmi na kuendelezwa harakati za kumfikia kila mtanzania kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa wale wenye kipato cha chini pia kuchangia vifaa na mahitaji mengineyo ya hospitali katika vijiji mbalimbali, kuongeza uelewa na ufahamu wa watanzania juu ya changamoto mbalimbali za afya na jinsi ya kukabili changamoto hizo mapema.

TAHMEF inatoa Shukrani za dhati kwa PSI na uongozi wote wa Mkoani Dodoma kwa ushirikiano mkubwa ulioleta mwitikio mzuri kwa wakazi wa kondoa na kufanikisha zoezi zima
 Wanawake wakazi wa Kondoa  wakipewa elimu juu ya Saratani ya shingo ya kizazi kabla ya kupewa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya Kizazi.
Wanawake wakazi wa Kondoa  wakisubiri kupewa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya Kizazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...