--
Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=.

kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/=

Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.

Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 wamepewa dhamana.

Mkuu wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bi.T. MNJAGIRA anawaasa Viongozi wote wa Umma, Wanasiasa na Watumishi wote wa Serikali, kuheshimu nyadhifa zao na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Pia, anatoa wito kwa  Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na  vitendo vya rushwa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria, Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumezuia vitendo hivyo visiendelee kujitokeza katika Jamii
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...