Wilayani Chamwino mkoani Dodoma maeneo karibu na Ikulu kunatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwa wakazi wa kijiji hicho na maeneo yanayokizunguka, ambapo linatarajia kufanyika Tamasha la 9 la muziki wa asili ya Cigogo 'Chamwino Music Festival'.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana mipangilio ya maandalizi kuelekea tamasha hilo yamekamilika kwa kiasi kikubwa yakiwemo makundi na kamati nzima ya maandalizi imekamilisha asilimia kubwa ya matakwa ya tamasha hilo.
Dk. Mapana anasema mipangilio imekamilika katika maeneo kama ukusanyaji wa fedha zitakazofanikisha tamasha hilo, maandalizi kwa washiriki na wageni waalikwa katika tamasha hilo.
Dk. Mapana anasema kwa upande wa bajeti ya tamasha hilo ambayo ilikuwa ni shilingi milioni 32 lakini zimepatikana milioni 18 kwa sababu kwamba wafadhili wakubwa ni watu binafsi wanaoamini urithi wetu ni muhimu sisi kama binaadam sababu utu wetu umejengeka katika mila na desturi.
"Ukitaka kupata utambuzi kwa wanachofikiria Wagogo jinsi wanavyokula, mahusiano yao ya kijamii na kwa ujumla kwa yote yanabebwa katika nyimbo na ngoma zao, hivyo tumeonelea tuyaweke wazi, ndipo tukaasisi tamasha hilo," alisema Dk. Mapana.
Anasema kwamba ufadhili wa tamasha hilo wameupata kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Chamwino Connect lenye makazi yake nchini Marekani huku wafadhili wengine ni serikali ya kijiji cha Chamwino ambacho kinatoa maeneo ya kufanyia tamasha hilo huku wafadhili wengine ni wasanii wenyewe ambao hujitolea kwa kiasi kikubwa ili kukuza utamaduni wao.
 Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana akimuonesha Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson matangazo ya tamasha
 Katibu Mtendaji wa Basata, Mngereza na Dk. Mapana wakiimba kwa pamoja mojawapo ya ngoma  katika tamasha la  Chamwino
Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana akipiga ngoma ya Kigogo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...