Kwa mara nyingine tena shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani limekuja na mambo mapya. Safari hii ni tamthilia ya mchezo wa redio unaofahamika kama Tamapendo. Lengo la tamthilia hii ni  kuonesha changamoto za vijana wawili kujiendeleza katika maisha yao katika jamii ambapo kanuni za unyanyasaji wa kijinsia za kijamii bado zinashinda.

Tamapendo inakuwa tamthilia ya pili ya redio kutengenezwa na shirika la UZIKWASA baada ya mchezo wa redio wa Penye Nia…..uliopatwa kusikilizwa na jamii nzima ya Pangani kupitia kituo cha redio cha Pangani FM, ambacho pia kinamilikiwa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani.

Shirika hili pia limekuwa na utaratibu kutengeneza filamu mbali mbali hasa kuhusu maswala ya haki na ukatili wa kijinsia.  Kutokana na utafiti wa ndani kabisa filamu za UZIKWASA zinasimulia story halisi  za jamii ya Pangani na zilifanikiwa kugusa watamazaji kwa sababu filamu hizi ni kama kioo cha changamoto zao.

Filamu hizo ni  Fimbo ya Baba ambayo ilitengenezwa mwaka 2006, Chukua Pipi iliyotoka 2012 na  filamu maarufu ya  AISHA ya mwaka 2015.  AISHA ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, siyo Pangani tu, lakini Tanzania nzima na nchi nyingi za kimataifa. Imepata tuzo mbalimbali kimataifa kutoka tamasha za filamu maarufu USA  na Africa.
Pamoja na hayo yote, sasa shirika la UZIKWASA limekuja tena na tamthilia la redio inayoitwa Tamapendo. Kama kawaidi ya filamu na tamthilia ya redio za UZIKWASA karibu waigizaji wote hutokea Pangani. Na ndivyo ilivyotokea kwa Tamapendo ambayo imeongozwa kwa ushirikiano na wagurugenzi wa mchezo Chande Omar na Irene Sanga. Story ya tamthilia hii inatokana na tafiti iliofanika na UZIKWASA pamoja na mchango wa wanajamii wa Pangani.  

Tamthilia imetengenezwa na kuhaririwa kwenye studio ya redio Pangani FM –Sauti ya Jamii.

Tamapendo ni kuhusu nini?

Ni story ya vijana wawili Fatuma na Chaballa wanaokutana na dhuruba kubwa ya maisha.  Wanajiona kuelemewa na mambo mazito kuhusiana na ukatili mbalimbali na dharau kuhusiana na haki za wanawake na wasichana.

Wakati wakijinusuru kutetea upendo wao wa dhati na kufuatilia ndoto zao katika maisha, wanajikuta kunaswa na mtego wa tamaa unaotawala kijijini kwao.  Je, unajua ni mtego gani waliokutana nao Fatuma na Chaballa?

Ni matumaini ya UZIKWASA kuwa  Tamapendo baada ya kuzinduliwa Pangani itazunguka nchi nzima ili kuwafikia wasikilizaji wengi na kuibua mijadala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...