Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea jana Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kufikwa na mauti inaelezwa kuwa marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake Mbagala Majimatutu jijini Dar es salaam mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika hospitali ya Rangi Tatu ili kupatiwa huduma ya dharura na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaalam iliyotolewa na madaktari inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi -  Amin.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.

IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...