Timu ya soka ya TPB Bank FC imefanikiwa kulipiza kisasi kwa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC baada ya kuifunga kwa mabao 3-2 katika mchezo huo maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sheria (Law School)  uliopo maeneo ya kituo cha mabasi cha Mawasiliano jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa kwanza, Taswa FC iliifunga TPB Bank FC kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja  huo huo.
TPB Bank FC ilitumia  idadi pungufu ya wachezaji wa Taswa FC kufunga mabao yote katika mchezo huo ambao pia ulikuwa wa maandalizi kwa timu hiyo ya benki kuelekea katika mashindano ya soka ya taasisi za kibenki yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Taswa FC ilianza mechi hiyo ikiwa na wachezaji nane tu.
Bao la kwanza la TPB Bank FC lilifungwa na nahodha wa timu hiyo, Baraka Kyomo  katika dakika ya 10 ya mchezo  baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Taswa FC na kufunga kirahisi.
 Wakati Taswa FC ikijiuliza, Kyomo alifunga bao la pili katika dakika ya 17 kabla ya Ojo Ajali kufunga la tatu katika dakika ya 35 ya mchezo.
Taswa FC ilianza harakati za kusawazisha mabao hayo kuanzia kipindi cha pili baada ya kutimia wachezaji wote 11. Bao la kwanza la Taswa FC lilifungwa na Fred Pastory baada ya kupokea pasi safi ya Zahoro Mlanzi kabla ya Shedrack Kilasi kufunga la pili kufutia mpira wa kona wa Juma Ramadhani.
Kiongozi wa timu hiyo Chichi Banda alisema kuwa wamefuraishwa na ushindi huo na kuwaomba Taswa FC kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata
 TPB bank FC
Taswa FC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...