Meneja Elimu kwa Mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Nchini (TRA), Bi. Dayana Masala ameongoza operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wa vituo vya mafuta wanaohudumia pasipo kutoa risiti na kusababishia serikali kutokusanya mapato stahiki kwa huduma wanazotoa  jijini Dar es Salaam. 
Operesheni hiyo ilifanyika mapema jijini humo na baadhi ya vituo vya mafuta kubambwa baadhi ya watoa huduma ya uuzaji wa nishati ya petroli na diseli wakitoa huduma ya kwa vyombo vya moto bila kutoa risiti kwa wateja jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi jambo linalosababishia serikali kupoteza mapato. 
Bi Msala amewaonya wafanyabiashara wenye tabia ya kutopenda kuwapa wateja risiti kwani kwa kufanya hivyo watalazimika watakapobainika watalipa faini ya shilingi milioni nne na nusu. Pia amewasisitiza wananchi kudai risiti wanapopata huduma za bidhaa mbalimbali kwani kwa kutokufanya hivyo pia ni kosa na wakikutwa wamenunua bidhaa bila kudai risiti watalazimika kulipa fidia ya shilingi milioni moja na nusu.
Imeandaliwa na Robert Okanda Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...