Cathbert Kajuna-Kajunason Blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungia vituo zaidi ya 10 jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuendesha biashara bila mashine ya Kielektroniki. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la kufungia vituo mbalimbali, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere amesema kuwa kwa sasa zoezi hilo linaendelea nchi nzima ili kuumbua vituo vyote vinavyokwepa kulipa kodi.

 "Tuliwapa muda wafunge mashine hizo mpaka mwaka jana 2016 mwishoni lakini mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo hivyo hatuna budi kuvifunga hivyo vituo mpaka pale watakapotekeleza matakwa ya serikali," amesema Kamshna Kichere. 

Kwa upande wa Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya amesema wakati umefika kwa wafanyabiashara kufuata makubaliano wanayokuwa wakiwafanya na TRA ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kwa sasa. Ameongeza kuwa sheria kali zitachukuliwa kwa wafanyabiashara wote ambao vituo vyao vya mafuta vimefungwa na wakakaidi. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (mwenye miwani kulia) akimuhoji msimamizi wa kituo cha GBP cha Sinza Mori jijini Dar es Salaam mara baada ya kufika kwa ajili ya zoezi la kukifungia kituo hicho kwa kukosa kuwa na mashine za kielektroniki. Wengine ni wafanyakazi wa TRA walioambatana nae.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (aliyenyoosha mkono) akiwahimiza vijana wake wafunge kituo hicho.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (kushoto) akiwa na  Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) wakitoa msisitizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...