KUWASILI kwa watalii 65 kwa treni inayoshikilia nafasi ya pili kwa ufahari duniani Rovos Rail, kumeendelea kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kama sehemu salama kwa utalii na mapumziko.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo katika kituo cha TAZARA jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devota Mdachi amesema fursa kama hizo zinapojtokeza ni wakati wao kuonyesha ukarimu wa watanzania.
“Sisi ndio wenyeji wao lazima tuonyeshe hawakukosea kuchagua kuja Tanzania, hivyo nawaasa wananchi kuwapa mapokezi mazuri na kuwakirimu wageni hawa ambao wengine watakwenda Zanzibar na wengine watabaki hapa kwa siku kadhaa kabla ya kuondoka,” alisema Bi. Mdachi na kusisitiza:
“Tanzania ina vivutio vingi, kama nilivyowahi kueleza siku za nyuma treni hii ambayo imeanza safari yake katika mji wa Pretoria Afrika wiki kadhaa zilizopita na kukanyaga reli ya TAZARA katika kituo cha Kapiri Mposhi nchini Zambia Julai 11, kisha ikakanyaga ardhi ya Tanzania Julai 12 imepitia vituo kadhaa vya kiutalii ikiwemo Mbuga ya Selous.”
TTB ipo katika mazungumzo na uongozi wa TAZARA ili kutumia nafasi ya wageni wanaotoka mataifa mbalimbali kujifunza utamaduni wa Tanzania pamoja na kutembelea vivutio vya kiutalii ili wanaporejea katika mataifa yao kuelezea uzuri wa nchi hii.
 Mkurugezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi akisalimiana  na mmoja wa watalii waliowasili Jijini Dar es salaam kwa treni kutokea Afrika ya kusini. Jumla ya watilii 65 wamewasili Tanzania kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. Hivi ni jitihada za TTB katika kutangaza vivutio vya utalii.

Mkuuwa Idara ya Masoko  wa TAZARA,Bwana Hemed Msangi(wapili kulia)akisalimiana na Meneja wa Treni ya Rovos Rail Bi. Daphne Mabala(kushoto) mara baada ya kuwasili na treni hiyo Jijini Dar es salaam ikiwa na watalii 65 kutokea Afrika ya kusini waliokuja kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya utalii Tanzania(TTB) Bi.Devota Mdachi. Hizi ni jitihada za Bodi ya utalii nchini katika kujitangaza.

 Watalii 65 wakishuka kwenye Treni  aina ya Rovos Rail jijini Dar es salaam wakitokea Afrika ya Kusini. Ikiwa ni jitihada za Bodi ya Utalii Nchini (TTB) na TAZARA katika  kufanikisha ujio wa watalii hao waliokuja kujionea  vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.
 Mmoja wa watalii kutoka Afrika ya Kusini akicheza ngoma ya kitamaduni ikiwa ni sehemu ya mapokezi kwa ujumbe wa watilii 65 waliowasili nchini kwa kutumia Treni aina ya Rovos Rail ambayo ni treni ya pili kwa ubora Duniani.

Mkuuwa Idara ya Masoko  wa TAZARA,Bwana Hemed Msangi(katikati) akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo walipotembelea na kuona mandhari ya Treni aina ya Rovos Rail ambayo ni treni ya pili kwa ubora Duniani ilipowasili Jijini Dar es salaam kutokea Afrika kusini ikiwa na jumla ya watalii 65 waliokuja kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini. 

Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...