BODI ya Utalii Tanzania (TTB), imeaamua kujikita kwenye utalii wa michezo na sanaa ili kuitangaza zaidi Tanzania kimataifa kupitia sekta hiyo inayojumuisha watu wengi ulimwenguni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari ya Dar es Salaam wakati akiwapokea watalii zaidi ya 50 raia wa Korea Kusini, Ofisa Habari Mkuu wa TTB, Bwana Geofrey  Tengeneza alisema imezoeleka watalii ni wale wanaokuja tu nchini na kutembelea maeneo ya vivutio na kuondoka, lakini hata wasanii na wanamichezo ni watalii wazuri wanaovutia raia wengine kutoka mataifa yao kuja Tanzania.
“Tumeamua kutumia mbinu hii ya kukaribisha watalii wa kimichezo na burudani kwa sababu kupitia wao watu wanaowafuatilia katika mataifa waliyotoka watavutiwa na Tanzania. Tumepoke wachezaji wa Haleluyah kutoka Korea Kusini. Wamewasili Juni 28 kupitia Zanzibar ambako waliweka kituo kwa wiki moja wakacheza mechi mbili na timu ya soka Polisi Zanzibar na Jang’ombe.
“Katika soko hili la Korea Kusini ni miongoni mwa mataifa tuliyoweka juhudi kubwa kupata watalii ikiwemo na China kutokana na idadi ya watu waliokuwepo,” alisema Bw. Tengeneza na kubainisha:
“Kazi yetu kubwa ni kutazama na kubuni mbinu za kuitangaza nchi yetu, wageni hawa zaidi ya 50 watakuwepo hapa kwa wiki moja, watakwenda Mikumi kisha Julai 8 watacheza mechi ya kirafiki na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.”
Akizungumzia ujio wao Kocha Mkuu wa Hallelujah FC, Bwana LEE Young Moo alisema wapo hapa kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu lakini pia wamevutiwa na utamaduni wa watanzania kutokana na sifa walizopata kutoka kwa watu waliotembelea taifa hili.
“Nafurahi kuwa hapa Tanzania tunataka kucheza na timu za Tanzania ikiwemo Yanga, tunataka kubadili utamaduni na kufanya kazi na wanamichezo wa hapa ili tuwe na uhusiano mzuri. Tumesika mambo mengi kuhusu Tanzania, kumbuka kuna mataifa mengi Afrika lakini utamaduni na watu wa taifa hili vimetuvutia sana,” alisema Bw. LEE.
Kwa upande wake daktari wa timu hiyo inayotajwa kuwa timu ya kwanza soka la kiushindani kuanzishwa Korea Kusini mwaka 1980 ambayo pia inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo, Bwana Benjamin Chang amesema anaamini wachezaji wake watakuwa na afya njema kutokana na hali ya hewa tulivu iliyopo Tanzania.
“Hali ya hewa ni nzuri, fukwe za kuvutia na naamini tutakuwa na wakati mzuri katika mbuga za wanyama. Tutakuwa hapa kwa wiki kadhaa tumekuja wachezaji 20 pamoja na maofisa wengine 30 jumla tupo 50, tumeona mambo mengi tuliyokuwa tukiyasikia tu,” alisema Bw. Chang.
Itakumbukwa miezi miwili iliyopita wasanii wa filamu zaidi ya 100 kutoka China walikuja nchini kufanya shughuli za kisanii na kutembelea vivutio ikiwemo fukwe za Zanzibar na mbuga za wanyama ikiwemo Serengeti.
Vilevile wiki iliyopita TTB ilipokea wachezaji 60 wa soka la wanawake kutoka mataifa 20 duniani walikuja kupanda Mlima Kilimanjaro na kucheza soka juu ya kilele cha mlima huo na kuitangaza Tanzania katika ulimwengu wa soka la wanawake.
 Picha ya pamoja ikionyesha kikosi cha timu ya soka ya Hallelujah FC inayoshirki ligi kuu ya Korea Kusini walipowasili Bandari ya Dar es Salaam wakitokea Zanzibar, timu hiyo ni sehemu ya watalii 50 waliotembelea nchini kuangalia vivutio vya kitalii na kucheza mechi za kirafiki ikiwemo na timu ya Yanga ya Dar es Salaam.
 Miongoni mwa watalii kutoka Korea Kaskazini waliowaili na kikosi cha timu ya soka ya Hallelujah FC, akicheza ngoma ya asili na mmoja wa wachezji wa kikundi cha Wanne Star katika bandari ya Dar es Salaam walipopokelewa na maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jana. Watalii hao watakuwepo nchni kwa wiki mbili kutembelea mbuga za wanyama na kucheza mechi za kirafiki ikiwemo na timu ya Yanga.
Mwanakikundi kutoka kikundi cha ngoma za asili cha Wanne Star, akicheza na chatu mbele ya watalii kutoka Korea Kusini walipowasili Bandari ya Dar es Salaam kutokea Zanzibar jana. Watalii hao waliopokelewa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) watakuwepo nchini kwa wiki mbili kutembelea mbuga za wanyama na kucheza mechi za kirafiki ikiwemo na timu ya Yanga.
Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...