Tumepata
taarifa kwamba kuna matapeli wamekuwa wakiwahadaa wanafunzi wanaoomba udahili
wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwapa taratibu zisizo
sahihi na kisha kuwaibia fedha zao.
Tunaomba
kuujulisha umma kwa ujumla kwamba udahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
unafanywa kwa kupitia mfumo wa kompyuta katika mtandao maalumu unaopatikana
katika tovuti iliyopo kwenye anuani: udsm.admission.ac.tz.
Maelezo ya jinsi ya kuomba udahili pamoja na habari nyingine za udahili
zinapatikana katika tovuti ya chuo yenye anuani: www.udsm.ac.tz.
Maombi
hayapokelewi kwa kujaza fomu. Pili, ada ya maombi ya udahili ni Shilingi
20,000/= tu ambazo zinalipwa kwa kutumia mitandao ya simu kwa kufuata maelekezo
yaliyowekwa kwenye mfumo wa udahili.
Tunatoa
pole kwa waliopata usumbufu na tunasisitiza umuhimu wa kufuata taratibu zilizo
rasmi katika zoezi zima la udahili.
Tunawatakia udahili mwema.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Shahada za Awali
Simu: +255222410069
+255222410751
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...