THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UFUTA KUUZWA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akutane na Bodi ya mazao mchanganyiko kwa ajili ya kuliondoa zao la ufuta na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Pia amewaagiza wakuu wa mikoa yote inayolima zao la ufuta kukutana na Dkt. Tizeba kwa ajili ya kupanga mfumo mzuri wa uuzaji katika msimu wa mwaka 2016/2017 wakati Serikali ikijipanga kuliingiza zao hilo katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017) wakati akisalimiana na wananchi katika vijiji vya Nangano, Kibutuka na Kiangara alipowasili katika wilaya ya Liwale kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi.

Ametoa kauli hiyo baada ya mbunge wa jimbo la Liwale, Mheshimiwa Kuchauka pamoja na wananchi kuiomba Serikali iwasaidie kuboresha bei ya zao la ufuta ambayo imekuwa ikiyumba.

Waziri Mkuu amesema “tatizo lipo kwenye mfumo wa  uuzaji zao la ufuta, unauzwa kwa bei ya rejareja, wanunuzi wako huru. Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuliondoa zao katika bodi ya mazao mchanganyiko na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuboresha bei yake.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Justine Monko kuhakikisha anamaliza tatizo la maji katika vijiji vya Nangano,Kibutuka na Kiangara.

Amesema  Serikali imedhamiria kuondoa tatizo la maji kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400. “Ndio maana Serikali imekuja na Kampeni inayosema mtue mama ndoo kichwani.”

Pia amemtaka Mhandisi wa Maji Bw. Andrew Kilembe kuandika barua ya kufuatilia fedha za maji sh. milioni 76 kwa ajili ya kijiji cha Kiangara walizopangiwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa Waziri wa Maji ili waweze kukamilisha uchimbaji wa kisima.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaeleza   wananchi wa Kijiji cha Kiangala  jinsi serekali ya awamu ya tano inavyo shughulikia kero za za wananchi Nchini Wananchi hao   walijitokeza July 10, 2017  ili waweze kumueleza kero  zinazo wasumbua  Waziri  yupo Wilayani Liwale Mkoa wa Lindi kwa ziara ya Kikazi ya siku Nne.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na Mkewe Mery Majaliwa wametembelea Hospitali  ya Wilaya ya Liwale July 10, 2017 na kuwapa zawadi  Watoto Mapacha wenye Siku Mbili  waliozaliwa katika Hospital ya  Liwale, Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa  wa Lindi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akihutubia umati wa wananchi wa  wilaya ya Liwale waliojitokeza kuja kumsikliza  Michezo wa  wilaya ya Liwale July 10, 2017 Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa wa Lindi.