Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 107.56 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Ipemba hadi Isongole wilayani Ileje yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa Songwe na Nchi jirani ya Malawi.

Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo amesema ujenzi huo utaanza mwezi juni Mwaka huu na kukamilka mwezi June, 2019.

“Tayari mkandarasi ameshapatikana na sasa ameanza kufanya maandalizi ya kuleta vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huu, Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kukamilisha ahadi hii kwa miezi ishirini na nne toka pale ujenzi utakapoanza”. amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amesema kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni katika hatua za kutekeleza ahadi iliyotolewa na Serikali kwa wanachi wa mkoa huu katika vipindi tofauti tofauti vya uongozi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akipata maeleozo ya mtandao wa ramani ya barabara za Mkoa wa Songwe kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM). 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipokea maoni ya mkazi wa wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM)  ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaanza mwezi juni Mwaka huu. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International ltd, Canada kuhusu kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara Mafinga-Nyigo KM 74.1 wakati alipokagua maendeleo ya mradi huo Mkoani Njombe. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...