Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kolobelo unashiriki  Mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland.

Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin umehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo  Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Swaziland, Botswana, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Botswana, Madagascar na Mauritius.Mkutano huo umeanza tarehe 8 Julai, 2017 na utamalizika tarehe 11 Julai, 2017.
 Waziri Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin akifungua Mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Swaziland.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki  mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland, kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kolobelo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...