THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

UPTADES msiba wa Professor Henslay William Kabisama, mazishi ni leo

Tunapenda kutoa taarifa kwa Ndugu, Jamaa, Marafiki, Familia na wote  tuliopatwa na msiba huu wa marehemu Professor  Henslay William Kabisama uliyotokea huko Ontario, California, Marekani. 

Mwili wa mpendwa wetu Prof Henslay Kabisama umewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana Ijumaa Julai 21, 2017 saa tisa mchana. Tunaombeleza nyumbani kwa marehemu Ursino  Victoria nyuma ya Ofisi za Halotel.  
Mazishi yatafanyika leo Jumamosi Julai 22, 2017 yakitanguliwa na Ibada ambayo itafanyika  katika kanisa la   St. Alban Upanga saa saba kamili mchana. Baada ya hapo tutaelekea  makaburi ya Kinondoni kwa mazishi. 

Bwana alitoa na bwana ametwaa
Jina la Bwana libarikiwe
AMEN.