Usaili
wa kuwatafuta washiriki wa mashindano ya kumtafuta mrembo wa Miss Grand
Tanzania utafanyika Julai 10, mwaka huu katika ukumbi wa Dar es salaam
Convention Centre, jijini Dar es Salaam.
Zoezi
za usaili litakalosimamiwa na wadau wa urembo nchini litaanza saa 4.00 asubuhi
na kufikia tamati saa 11.00 jioni.
Mratibu
wa mashindano hayo nchini Abraham Mahimbo amewataka warembo wenye vigezo
kuichangamkia fursa hiyo kwani ni mashindano yanayokuja kuleta mapinduzi katika
fani ya urembo nchini.
Mahimbo
amesema mashindano ya Miss Grand Tanzania ambayo yatakuwa chini ya Miss Grand
International yanakuja kuleta mapinduzi na kuyapa heshima mashindano ya urembo
nchini.
“Warembo
wanaojiamini na waliotayari kwa mapinduzi ninawakaribisha katika usaili kwani
nafasi hii ni adhimu ambayo hutokea mara moja tu katika maisha,” alisema
Mahimbo.
Amevitaja
vigezo vya kushiriki mashindano hayo ni umri wa kati ya miaka 18-27, urefu sentimita
168, ambaye hajaoelwa, hajawahi kupata mtoto, ajue
utamaduni na matukio yanayoendelea nchini, kisiasa, uchumi, mazingira, matatizo,
awe na tabia njema na hajawahi kujihusisha na vitendo vya aibu kama biashara ya
ngono.
Alisema
siku ya usaili washiriki watatakiwa kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa na fomu
zinapatikana Swahili Studios- Magomeni, Merry Bright Beauty Point-Tabata, City
Star Boutique- Namanga na Infinity Lounge Mbezi Beach.
“Kwa
mawasiliano kuhusu ushiriki wa mashindano hayo wawasiliane nami kwa namba ya
simu 0717 653 653.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...