Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo leo amekutana  na timu itayotekeleza mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu katika kikao  kazi  kilichofanyika ofisini kwake jijini Arusha.
 Mhe Gambo ameshauri wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kuwa makini katika masuala ya ajira hasa zile za vibarua kwani mara nyingi zinaleta malalamiko kwa serikali, hivyo amewataka kuwa makini katika kufuata taratibu za ajira za vibarua.
Mkuu wa Mkoa huyo pia amemshauri mkandarasi kua makini na 'sub contractors' wanaowapa kazi kazi mara nyingi wamekua wanafanya utapeli wa kuchangisha wananchi hali inayopelekea kuichafua serikali hususani Shirika la Umeme Tanesco.
"Mara nyingi watu mnaowapa kazi wanakua wanafanya vitendo vya kitapeli kwa wananchi, kwani wanakua wanapita na kuchangisha wananchi michango ambayo kimsingi ni makosa mfano wanaweza kuwaambia wananchi wachange hela ya nguzo ama kuchimba mashimo ya nguzo,nendeni mkakemee vitendo hivyo" alisema Mhe. Gambo.
Mradi huo unategemea kuanza mapema mwezi Agosti na utatekelezwa katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha ambao una changamoto kubwa ya  umeme.

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo katika kikao kazi  na timu itayotekeleza mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu  ofisini kwake jijini Arusha leo.
 Wajumbe wa kikao kutoka kushoto ni Rama Shankar na Abas Kitola wa Angelique Int. Ltd, Eng. Donasian Shamba wa TANESCO Arusha na Eng. Gaspar Msigwa  ambaye ni Meneja TANESCO Arusha
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho kutoka kushoto ni Chuwa African wa TANESCO Arusha, Wilson Chilewa na Kurwa Nelson wa NIPO Group Ltd.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...