Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi ametoa ushauri kwa kina mama hususani wasichana kutumia vipodozi vyenye vimea asilia ili kuepukana na kuharibu ngozi zao.
Amesema hayo wakati akiongea na globu ya Jamii, Irene amesema kupitia saluni ya Timeless wameweza kuwasaidia watu wengi na kuwapatia tiba kuhusiana na masuala ya ngozi na hasa katika usahihi wa kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi ya muhusika.
"Tunatoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipodozi kulingana na aina ya ngozi ya muhusika pia kutoa malekezo ya kutumia vitu sahihi kwa wakati sahihi kama vile kulingana na hali ya hewa kipindi cha joto na baridi,"amesema Irene.
Amesema kuwa, anatoa ushauri kwa vijana hususani wa kike kujifunza zaidi masuala ya urembo kwani inaweza kusaidia katika kuboresha ngozi zao na wanaweza kutumia vipodozi sahihi na kutokuharibu ngozi zao.
Mbali na kutoa tiba, Timeless walianza kutoa mafunzo rasmi mwaka 2016 Irene amesema kuwa wanatoa mafunzo kwa vijana wanaopendelea kufahamu shughuli mbalimbali za urembo ikiwemo tiba ya ngozi, upambaji ambapo wameweza kutoa vijana wengi kwa kipindi cha mwaka mmoja na tayari wengine wameshajiajiri katika sehemu zao na pia Timeless wanajishughulisha na masuala ya kupamba maharusi, nywele na kucha na mapambo ya maharusi ikwemo kadi.
Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akimuhudumia mteja aliyetembelea katika banda lao la Timeless Hair and Beauty Saloon kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

 Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akizungumza na Globu ya Jamii kuhusiana na masuala ya urembo wa ngozi na kuonyesha baadhi ya mapambo ya maharusi yanayopatikana kwenye saluni yao ya Timeless.
Wateja wakiwa wanapata maelezo kutoka kwa  mfanyakazi wa Timeless Hair and Beauty Saloon katika banda laokwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.Picha na Emanuel Massaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...