NA BASHIR NKOROMO, DAR.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi leo ametangaza rami tarehe ya Wanachama wa Jumuia hiyo kuanza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi tangu ngazi ya Kata hadi Taifa, na kusema fomu zinatolewa bure, huku akionya kuwa atakayejaribu kutumia rushwa kuomba nafasi yoyote atakatwa.

Pia ametumia ameaema UWT inaunga mkono tamko la Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli alilolitoa hvi kribuni kwamba, ni marufuku kwa msichana atakayepata ujauzito akiwa shuleni katika mfumo rasmi kurudi masomoni katika mfumo huo rasmi.

Makilangi amesema, UWT inaunga mkono tamko hilo kwa sababu ndiyo maelekezo yaliyomo katika Ilaniya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, na pia ndiyo Sera ya Serikali katika kusimamia utoaji elimu katika mfumo rasmi hapa nchini.

"Tafiti mbalimbali za Jumuia na Taasisi nyingine hapa nchini na za Kimataifa likiwemo Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataida (UNICEF), Mwanafunzi mjamzito au aliyejifungua ni vigumu kuendelea na masomo katika mfumo ambao umeandaliwa kulingana na Saikolojia ya akili ya mtoto asiye na majukumu ya malezi na ndiyo maana upomfumo uliopendekezwa na sera na ilani ya CCM kwamba anayekatiza masomo katika mfumo rasmi anaweza kuendelea katika mfumo usio rasmi, Mifumo isyo rasmi kwa ajili ya wanafunzi wa aina hiyo na wengine waliokosa masomo katika mfumo wa kawaida ni  kama MEMKWA na QT" , alisema Makilagi.

Alisema UWT inatambua na kuheshimu mapendekezo  ya tafiti hizo kuhusu watoto na pia inakubaliana na sera ya Serikali na Ilani ya CCM kuweka utaratibu bora na wenye manufaa  zaidi wa kuwazuia wajawazito na wazazi  kuendelea na masomo katika mfumo rasmi na badala yake kutengeneza mfumo mbadala wa kupata elimu kwa kuwa kufanya hivyo kumaimarisha nidhamu, na uwezo wa kitaaluma wa watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...