SHIRIKISHO la Riadha la Taifa (RT) limezitangaza rasmi mbio za Rock City Marathon kuwa mbio za kimataifa baada ya kukidhi vigezo vyote ikiwa ni pamoja na kuhusisha mbio za km 42 kwa mara ya kwanza. Hatua ambayo imepongezwa na wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, na Kagera kwa kuwa itachochea ukuaji wa utalii katika kanda hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha mbali na kupongeza hatua hiyo alisema uwepo wa mbio hizo katika kalenda ya Riadha kimataifa itawavutia watalii wengi katika ukanda huo pia na hivyo kufungua fursa zaidi kupitia utalii.

“Tunatarajia kwamba sasa mbio hizi zitafahamika zaidi duniani na kuvutia washiriki wa kimataifa ambao tunatarajia pia watakuja kama watalii na pia watapata kufahamu fursa za kiuwekezaji,’’ alisema.

Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International. 
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rock City marathon mwaka 2017 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi (kulia) aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi (wa pili kushoto) na Makamu wa pili wa Shirikisho la Riadha Taifa (RT), Dk Hamad Ndee. Bi Tesha alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack akitoa nasaa zake kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Rock City Marathon uliofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba  jijini Mwanza kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International.
Mpimaji wa njia wa njia za riadha anayetambulika kimataifa Bw John Bayo akimuonyesha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa njia zitakazotumika katika mbio hizo baada ya kupimwa kitaalamu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye uzinduzi huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...