KATIKA kuadhimisha siku ya kuzaliwa rais wa kwanza mzalendo wa  Afrika Kusini, Marehemu  Nelson Mandela,  vijana kutoka Mpango wa Viongozi Vijana wa Afrika (YALI), wamepanda miti 50 katika Shule ya Msingi Mapambano, Wilaya ya  Kinondoni, jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana diwani wa Kata ya Sinza, Bwana Geoffrey Chikanamwali, amesifu kitendo cha vijana hao kuwa ni  cha kuigwa na kuongeza kuwa  dunia   sasa inahitaji miti zaidi ili kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Amekihimiza kikundi hicho kupanda miti zaidi katika maeneo mengine ya nchi ili kuleta mabadiliko kama alivyofanya Mzee Mandela ambaye jana walitambua mchango wake.
“Leo tumechagua eneo la shule lakini nashauri mpande miti ndani na nje ya Dar es Salaam ili kupambana na hali ya hewa ya ukaa inayoharibu dunia yetu,” alishauri Bw. Chikanamwali.
Mwalimu Mkuu  Abdallah Ndalakaa amesema shule hiyo imewakilisha shule nyingine za Tanzania katika tukio hilo na kusema vitendo vya kizalendo vilisishwe kwa vizazi vijavyo. Marehemu Mandela na viongozi wengine wa Afrika walipambana na ukoloni na udhalimu kwa sababu ya uzalendo, amesema. Mandela alifungwa na makaburu kwa miaka 26.
Mwakilisha wa YALI, Bibi Wingila Mpamila anayesoma Shahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, amesema wamechagua kupand miti kwani ni kipindi  ambacho dunia inapambana na mabadiliko ya kimazingira.
“Watu wanakata miti hovyo, tumeamua kutumia siku hii ili kuonyesha mfano kwa vijana wengine duniani kuokoa mazingira. Tumejitoa kama alivyojitoa Mzee Mandela kutoka moyoni bila kutegemea malipo,” alisema Bi. Mpamila.
Julai 18, ni siku ya kuzaliwa Nelson Madiba Mandela na uazimishwa na watu wanaothamini mchango wake.
Diwani Kata ya  Sinza  Mhe. Godfrey Chikandamwali  akipanda mti  katika Shule ya Msingi Mapambano  Sinza jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku  ya Mandela  (Mandela day) inayoadhimishwa Julai 18 kila mwaka duniani. Zoezi  hilo limeratibiwa na Mpango wa Viongozi Vijana wa Kiafrika(YALI) ikiwa ni moja ya shughuli za mpango huo.
 Diwani wa  Sinza  Mhe. Godfrey Chikandamwali  (katikati waliokaa)akiwa na  Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Msingi Mapambano  Bwana  Abdallah Ndalakaa(kushoto kwake) pamoja na wazazi na  wanachama wa Mpango wa Viongozi Vijana wa Kiafrika (YALI).  Kwenye maadhimisho ya siku  ya Mandela  (Mandela day) inayoadhimishwa Julai 18 kila mwaka duniani. YALI waliratibu Mpango huo kwa kupanda miti   katika Shule ya Msingi Mapambano  Sinza jijini Dar es Salaam. 
Wanachama wa Mpango wa Viongozi Vijana wa Kiafrika (YALI). Wakishirikiana na wanafunzi wa  Shule ya Msingi Mapambano kupanda  mti katika maeneo ya shule hiyo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku  ya Mandela  (Mandela day) inayoadhimishwa Julai 18 kila mwaka duniani. YALI imesimamia zoezi hilo ikiwa ni moja ya shughuli za Mpango huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...