Na Dotto Mwaibale
VIONGOZI wa dini wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kumsaidia Rais Dk. John Magufuli kuliletea taifa maendeleo na kuondokana na umaskini nchini.
Mwito huo umetolewa na muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu wakati akihubiri katika kongamano la kimataifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es Salaam leo.
Alisema viongozi wa dini waliopo katika makanisa wanataaluma mbalimbali hivyo mbali ya kuhubiri neno la mungu wanapaswa kutumia taaluma walizonazo kumsaidia Rais katika maendeleo ya nchi jambo litakalosaidia nchi kuondokana na umaskini na adui ujinga.
Dk.Kyungu alisema katika imani Tanzania sasa imetoka katika uchanga na sasa inakwenda mbele na hilo ni jambo la kujivunia.
Alisema nchi ya Tanzania imebarikiwa tangu uongozi wa baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa Dk. John Magufuli.
"Ili ni jambo la kujivunia kwa nchi kuwa na amani tangu wakati huo hadi leo hii na ndio maana tumeona ni vizuri tukafanya maombi ya shukrani ya kuliombea taifa na Rais wetu yatakayofanyika Jumamosi Uwanja wa Uhurua jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi" alisema Dk. Kyungu.
 Muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu  akihubiri katika kongamano la kitaifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi  Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

 Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Dodoma, akifundisha katika kongamano hilo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maombi hayo, Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church, Dk.David Mwasota akizungumza katika kongamano hilo.

 Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria alifundisha somo la watu kuwa waaminifu katika kila jambo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...