Mpango mpya unaohamasishwa na wadau wa sekta ya kilimo hatimaye utawapa wakulima wadogo nchini kote fursa ya kupata masoko ya uhakika na endelevu kwa kuepuka madalali wa mazao yao.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Farm Africa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Tanzania wa Farm Africa,  Steve Ball alisema kuwa warsha hiyo ililenga kuwafudisha wakulima namna bora kuingia kwenye mfumo rasmi wa biashara ya nafaka.

Alisema kuwa jukwaa hilo la wadau kwenye sekta hiyo linaunganisha biashara nzima ya nafaka kutoka kwenye shamba hadi sokoni  na inashirikisha mkusanyiko wa programu zinazoruhusu watumiaji kusimamia hesabu, mazao ya biashara, soko endelevu na kupata mikopo kutoa kwenye taasisi za fedha.

"Tuko hapa kuzungumza juu ya njia bora ya kuwasaidia wakulima wadogo ili kuepuka madalali wakati wa kutafuta masoko ya mazao yao na ili waweze kupata kwa bei bora zaidi baada ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka juu ya mwenendo wa soko,” alisema.

Aliongeza pia kwamba wadau katika sekta hiyo wana matumaini kwamba wakulima watakusanya nguvu kwa pamoja na kutengeneza maghala yao ya kuhifadhi mazao yao na kuuza kwa pamoja ili kupata bei nzri zaidi.

Alibainisha kuwa kwa njia ya G-Soko, wakulima wanaweza kuunganisha mavuno yao kupitia ghala lao na kuthibitishwa na kupata huduma za kifedha kwa kutumia nafaka zao kama dhamana. Jukwaa pia hutoa programu ya malipo ya huduma na ukusanyaji wa data wa wakulima.


Mkurugenzi Mkazi wa Farm Africa, Steve Ball akizungumza kuhusu umuhimu wa wakulima kupata taarifa za uhakika kuhusu mwenendo wa masoko, wakati wa warsha ya wadau wa mazao ya nafaka iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...