Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, amewataka manahodha na mabaharia wa meli ya MV. Liemba kufanyakazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuiwezesha meli hiyo kujiendesha kibiashara.

Akizungumza na wafanyakazi wa meli hiyo Prof. Mbarawa, ameelezea kuridhishwa na mabadiliko yanayoendelea katika meli hiyo na kuwataka wasibweteke bali waongeze ubunifu.“Hakikisheni mnatoa huduma bora kwa wateja wenu na kupata faida ili serikali na wadau wengine wawaamini na kutumia huduma yenu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ameitaka meli hiyo kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi ili kuhuisha huduma za usafiri na uchukuzi katika Ziwa Tanganyika. 

Prof. Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya ukaguzi wa miundombinu mkoani Kigoma amepata fursa ya kukagua utendaji wa meli ya MV. Liemba, kupata chakula cha pamoja na wafanyakazi wake katika meli hiyo na hatimae kutoa maelekezo kwa manahodha na mabaharia wa meli hiyo kongwe hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata chakula na manahodha na mabaharia wa meli ya MV Liemba inayofanya safari katika Ziwa Tanganyika.
Muonekano wa meli kongwe ya MV. Liemba ikiwa imetia nanga katika bandari ya Kigoma, meli hiyo imeatkiwa kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...