WAZIRI wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga amesema wanafunzi wahitimu kutoka vyo vya nje ya nchi waunde umoja wa mataifa waliyotoka ili kuwa na jukwaa la kuvuna wataalamu pamoja na wao kutambuana.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizindua Chama cha wanafunzi waliosoma China (CAAT), jijini hapa ambapo alibainisha vyama vingi vya aina hiyo vimeanzishwa na kupotea kutokana na kukosa msukumo kutoka serikalini.
“Nyinyi mtakua kiungo kati ya wasomi kutoka China, serikali na jamii, hiki ni chama cha kwanza cha wanafunzi waliosoma  China. Matarajio yangu ari iliyowafanya kujipanga pamoja itabaki daima na naamini chama hiki kitakua jukwaa la wanafunzi wanaoendelea kusoma na waliohitimu,” alisema Balozi Mahiga.
Aliongeza kuwa: “Najua kuna Wachina nchini walioanzisha viwanda na wangependa kupata vijana wasomi, hii ni fursa pekee ya kuendeleza sekta binafsi na kudumisha urafiki wetu. Ningeshauri idara za serikali na sekta binafsi kuwa karibu na chama hiki.
“Nimezungumza nao na nimeona aina ya utaalamu waliokuwa nao, utaalamu huu utasaidia kuleta tija kwa idara mbalimbali na wizara pamoja na taasisi za umma. Nitaangalia namna wizara yangu itakavyokisaidia chama hiki ili tusiwaache peke yao ubunifu waliofanya ni wa ahali ya juu kabisa.”
Balozi  msaidizi wa China nchini, Bw.

 Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine Mahiga Wa kwanza (kushoto) ni  Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong  wa pili (kulia) ni  Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana. Mbelwa Kairuki wakinena jambo kwenye  hafla  fupi ya kuzinduzi wa Ofisi za umoja wa wahitimu Wanafunzi   Watanzania walio Soma nchini China au China Alumni Association of Tanzania(CAAT) iliyofanyika
jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine akinena jambo na  Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye hafla  fupi ya kuzindua Chama cha umoja wa wahitimu, Wanafunzi    Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT)  jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine akiambatana  na  Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye uzinduzi wa ofisi za  umoja wa wahitimu, Wanafunzi  Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) ) iliyo fanyika Posta  jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine Katikati akipata picha ya pamoja na  wanaumoja wa (CAAT)  wapili (kulia) ni Balozi wa Tanzania Nchini China Bwas.  Mbelwa Kairuki  wa kwanza (kushoto) ni Mwenyekiti wa  (CAAT)  DKT.Liggy Vumilia  wa pili (kushoto) ni Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye  hafla  fupi ya kuzindua Ofisi za  Chama wa wahitimu, Wanafunzi   Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) iliyo fanyika  jijini Dar es salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...