THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WANADAYASFORA WA MAREKANI WATOA HUDUMA ZA MATIBABU ZANZIBAR


Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 03-07-2017

Wananchi wa Tanzania wanaoishi Marekani wanadiaspora wakishirikiana na Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.

Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema wameamua kuja nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali.

“Tumekuja Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali mbali na kuwapatia matibabu kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health Education Development kwa kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure pamoja na maradhi ya akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani Bi. Asha Mustafa Nyang’anyi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu ujio wao hapa Zanzibar.
Bwana. Amiri Muhammed Amiri akimuonesha fangas Daktari bingwa wa ngozi Mamotheo alipokuwa akitoa matibabu katika hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. 
Baba wa mtoto Abdulmajid akiwaonesha madaktari bingwa wa maradhi ya ngozi namna mwanawe alivyodhurika kwa kufanya mabaka mwilini katika hospitali ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.