Na Mwandishi Maalumu, Lufilyo 
Jana, Jumamosi tarehe 22 Julai 2017 ilikuwa siku ya kipekee familia ya Profesa Mwark Mwandosyak kwani Wananchi wa Busokelo walifanya tafrija pale Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, ya kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. 
Akiwa amehemewa na tukio hilo, Profesa Mwandosya alisema hiyo ni heshima iliyoje kwake, Mke wake Lucy Akiiki, watoto wao; Max Mwandosya, Sekela Mwandosya, Emmanuel Mwandosya, na wajukuu Tusekile, Lusekelo, na Queen Maria, Mkwe Digna Mwandosya, na ndugu na marafiki wa karibu. 

Katika risala iliyosomwa kwa niaba yao na Mwalimu Juma Mwakikuti, Mwalimu Mkuu wa Seminari ya Manow, Wananchi wa Busokelo, au Rungwe Mashariki kama Jimbo lilivyojulikana kabla ya kuwa Halmashauri kamili, walishukuru kwa kile walichoona kama mchango mkubwa alioutoa katika maendeleo ya Busokelo, Rungwe, Mbeya na Tanzania kwa ujumla, katika kipindi ambacho Profesa Mark Mwandosya alikuwa Mbunge wao. 

Waliorodhesha mambo mengi ikiwa ni pamoja na: elimu; afya; mawasiliano; miundombinu; utamaduni; utawala (kuanzishwa kwa Halmashauri); maji safi karibu kila kijiji; umeme kila kata kuanzia mwaka 2002; mshikamano wa Jimbo; michezo; Kituo cha Utamaduni, Mila, Historia, na Desturi za Wanyakyusa; Benki ya NMB; Ujenzi kupitia Shirika la Nyumba la Taifa; na kadhalika. Kipekee walimshukuru Mama Lucy Mwandosya kwa kulea watoto yatima na kuwasomesha kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu, na kujenga kituo cha ufundi cha watoto hao ambacho amekikabidhi kwa Serikali na sasa kimekuwa Chuo cha Ufundi cha VETA. 
Mzee Mwakihwanja kutoka Lupata akimvishaProfesa Mark Mwandosya wakati wa tafrija maalumu ambayo  Wananchi wa Busokelo waliandaa jana Jumamosi Julai 22, 2017 ili kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015, Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, mkoani Mbeya mgolole Profesa Mark Mwandosya wakati wa tafrija maalumu ambayo  Wananchi wa Busokelo waliandaa jana Jumamosi Julai 22, 2017 ili kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015, Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, mkoani Mbeya.

Profesa Mark Mwandosya akifurahia zawadi yake ya mkuki na mgolole
Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Jumamosi,tarehe 22 Julai 2017 kwa heshima ya Profesa Mark Mwandosya baada ya Wananchi wa Busokelo kuandaa  tafrija Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, ili kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...