THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Watanzania waaswa kutembelea hifadhi ya Wanyama ya Ngorongoro

Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) anayeshughulikia huduma za jamii, Asangye Bangu amewataka watanzania kuanza kuhamasika kutembelea hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro ili kujionea mambo mbalimbali yanayopatikana ndani ya hifadhi hiyo.

Bangu amesema hayo akiwa katika banda la balozi wa hifadhi hiyo Mrisho Mpoto lililopo katika viwanja maonesho ya biashara vya Babasaba jijini Dar es salaam.

“Hii ni fursa ya pekee kwa watanzania kuanza kuhamisika na kwenda kuangalia maajabu ya hifadhi ya Ngorongoro, kusema kweli tunakosa uhondo kabisa. Kwa sababu wewe jiulize mzungu anapanda ndege na kutumia gharama kubwa kuja Ngorongoro wakati sisi wenyewe tupo karibu hapa tunashindwa kuwapeleka watoto wetu kijifunza mambo mbalimbali,” alisema Bangu.

Alisema Ngorongoro Crater ni mbuga ya wanyama mfano wa bakuli kubwa lililoundwa miaka 25 elfu iliyopita baada ya milima miwili Makaroti na Satiman kulipuka na kutoa tope lenye moto. Tope hili ndilo lilikuwa na tabaka tatu za udongo na kuumba bonde lililofanana na bakuli kubwa ambalo wenyeji wa kabila la Kimasai walilipa jina la Ngorongoro Kaldera.

“Kijiji cha Malanja ni cha pekee katika bonde la Ngorongoro katikati ya Milima ya Makaroti ambao ni mkubwa na Satiman ambao ni mdogo. Wenyeji wa kijiji hicho huendesha Maisha yao kama kawaida ya kufuga mifugo yao ndani ya mbuga wakichanganyika na wanyama pori,” alisema

Pia katika bonde hilo kuna mto mmoja ambao unatoka Olmot Crater, Ziwa Magadi ambalo wakati wa kiangazi hukauka na kutoa vumbi aina ya majivu ambayo wenyeji wa Kimasai hutumia kuwalisha Ng’ombe kama dawa ya kudhibiti magonjwa.

Alisema huwezi kuitaja Hifadhi ya Ngorongoro Crater bila kuwataja wanyama wakubwa wajulikanao kama “Big Five”, ambao ni Faru, Tembo, Chui, Nyati na Simba.

“Kinachovutia zaidi ni kuona wanyama wote, wakali na wapole jinsi wanavyoishi kwa pamoja hadi pale tu wanapokuwa na njaa ndio hubadilikianana. Penye kundi la Nyumbu, Faru, Punda milia, Ngiri, Nguruwe na kadhalika utawakuta pia Simba pembeni wamelala wakipunga upepo baada ya kupata mlo wa mchana. Hii ni kuonyesha kwa jinsi gani wanaishi kama familia moja na wako katika nyumba moja,” alisema B

Bangu aliwataka watanzania kuacha kusimuliwa kuhusu ufahari wa Ngorongoro bali watembelee mbuga hiyo kwaajili ya kujionea wenyewe