Na Sixmund J. Begashe  wa Makumbusho ya Taifa
Watanzania wameshauriwa kuunga mkono jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali, Mashirika ya Umma na Wadau mbali mbali katika mapambano dhidi ya rushwa  ili kutokomeza kabisa tatizo hili hapa nchini. 
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bwana Achiles Bufure kwenye usahili uliofanywa na Makumbusho hiyo ili kuchaguwa wasanii watakao unda kikundi kimoja kwa lengo la kutoa elimu ya Mapambano dhidi ya Rushwa hapa nchini.
 Bw Bufure ameongeza kuwa Makumbusho imeona itumie wasanii wa fani mbali mbali kupitia program ya sanaa na Utamaduni ijulikanayo MUSEUM ART EXPLOSION ili kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi na ambao utakaokaa akilini mwa watu kwa muda mrefu kupitia sanaa za ufundi na zile za jukwaani. 
Wakizungumza baada ya Usahili huo, msanii Bi Yame Muhamedi wa Kikundi cha sanaa cha UKOO na Salum Mbaya wa St Kamilius Wameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuwashirikisha wasanii katika program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION kwani  imewapa nguvu na hari ya kuendelea kufanya kazi za sanaa katika kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo ndani ya nchi na kuahidi kufanya vyema kazi iliyopo mbele yao ya kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya madhara ya Rushwa nchini. 
Program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST COTTUPTION ni moja kati ya program tano nchini zilizopata ufadhili wa Ubalozi wa Uswiss wenye lengo la kutoa elimu kwa watanzania juu ya Madhara na namna ya kupambana na Rushwa nchini.
 Wasanii kutoka vikundi mbali mbali wakifanya usajili kabla ya usahili.
 Wasani wakiwajibika katika usahili uliofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam ili kupata nafasi ya kushiriki mapambano dhidi ya rushwa kupitia sanaa.
 Usaili ukiendelea jukwaani
Kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw. Achiles Bufure akifuatilia kwa karibu zoezi la usahili kwa wasanii  lililofanywa na Makumbusho hiyo. Kulia ni Msanii Nguli wa sanaa za Jukwaani Bw Aloyce Makonde akitoa maelezo kwa wasanii  wakati wa usahili huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...