Na Tiganya Vincent

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linawashikiria watu watatu kwa tuhuma za mauaji  ya Bwana Mahona Pondamali (50)  mkazi wa Wilaya ya Sikonge yanayosadikiwa kutokea Aprili mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema mnamo tarehe 22 mwezi wa nne mwaka huu mke wa marehemu aliripoti Polisi kupotea kwa mme wake katika mazingira ya kutatanisha na ndipo Jeshi la Polosi ilopoamua kuanza uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kubaini kuwa mtu huyo akupotea bali aliwawa.

RPC Mtafungwa alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio kuwa marehemu alipokuwa akinywa pombe alikuwa na tabia ya kumpiga mke wake na watoto na ndipo walipoanda mpango wa kumkodi  mtu wa kumpiga kwa ajili ya ya kumrekebisha tabia hali iliyosababisha mauti yake.

Alisema kuwa baada ya wahusika kubaini kuwa marehemu amekufa ndipo walipoamua kwenda kumtupa katika shimo la wachanaji mbao.

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi kwa kushirikiana na wananchi ndipo walipo gundua kuwa marehemu yuko katika shimo la wachana mbao  na kuamua kulifukua ndipo ndugu wa marehemu waliposema kuwa  ni ndugu yao aliyedaiwa kupotea

Aliwataja wanaotuhumiwa wanaoshikiriwa na Polisi kwa uchunguzi kwa tuhuma za mauaji kuwa Mke wa Marehemu Bibi Tatu Said(30) , mtoto wa marehemu Katambi Mahona (13)na jamii wa kukodi Mwanza Mburuka(31).

Kamanda Mtafungwa aliongeza katika tukioa hilo Polisi walifanikiwa kukamata ng’ombe mmoja  kwa Mburuka ambaye inasadikiwa kuwa ujira kwa mauaji hayo  na jeshi hilo linaendelea kumchunguza kama kuna amekuwa akikodisha ili kutekeleza mauji mablimbali mkoani hapa.

Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...