Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa Victoria na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania( Tanzania Albinism Society -TAS) wamefanya usafi wa mazingira kisha kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.

Katibu Mtendaji wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS Taifa Bw. Mussa Mussa akizungumza katika kituo/Shule ya Msingi Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele.Kushoto ni Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe.

Watoto na maafisa kutoka TAS wakiwa eneo la tukio
Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale akila chakula na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...