Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa Victoria na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania( Tanzania Albinism Society -TAS) wamefanya usafi wa mazingira kisha kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.

Watemi hao wakiongozwa na Katibu Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza walitembelea kituo hicho leo Jumamosi Julai 8,2017. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba alisema chama hicho kimekuwa na ushirikiano mkubwa na machifu wa kanda ya ziwa hicho kuamua kushiriki nao katika kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha Buhangija. 

“Malengo ya kuja hapa kwanza ni kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kuhusu masuala ya usafi,pili ni kuwapa ujumbe watoto hawa kuwa wawe na utamaduni wa kufanya usafi hata wanaporudi kwenye familia zao,tatu tumekuja kula chakula cha pamoja na watoto hawa ili kuonesha kuwa tuko pamoja nao”,alieleza Temba. 

Temba alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuchunguza utitiri wa mashirika yaliyoanzishwa nchini ambapo sasa yapo zaidi ya 10 na kufuatilia vituo mbalimbali vilivyoanzishwa kwa lengo la kuwahudumia watu wenye ualbino hususani watoto kwani sasa vipo takribani 20 lakini wahusika wa vituo hivyo hawasaidii walengwa. 

Temba alisema mashirika mengi yamekuwa yakijikita katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino huku yakisahau kuwa watu wenye ualbino wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikiua watu wengi wenye ualbino. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba,Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu na Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga wakila chakula na watoto kituo cha Buhangija.

Katibu Mtendaji wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa,Mussa Mussa akizungumza katika kituo/Shule ya Msingi Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele.Kushoto ni Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale akizungumza katika kituo cha Buhangija.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba 
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliiomba serikali kuona umuhimu wa kuwapa nguvu viongozi wa kimila kama zamani kwani wanazungukwa na watu wengi hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii.
Watoto,walimu na maafisa kutoka TAS wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...