Na. Paschal Dotto- MAELEZO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Janauary Makamba amewaasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha kupata utaalamu katika fani ya uhandisi.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais katika Tamasha la Wahandisi wanawake(TAWECE) lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salamu Mhe. Makamba amesema kuwa katika juhudi za kujenga taifa la viwanda fani ya uhandisi ni muhimu hivyo watoto wakike hawana budi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi.

“katika hali ya kawaida wahandisi wa kike ni wachache kulinganisha na wahandisi wa kiume hii ni kutoka na kuwepo kwa imani kuwa masomo katika kada hii ni ya wanaume na si wanawake kama watoto wengi wanavyojua,watoto wa kike onyesheni tofauti someni masomo ya sayansi muweze kutoa mchango kwa taifa “ Alisema Waziri Makamba.

Pia Waziri Mhe. Makamba ameishukuru Serikali ya Norway kwa kutoa nafasi kwa masomo kwa watoto wa kike kusomea uhandisi kwani hali hii imesaidia kuongeza idadi ya wahandisi wa kike kutoka 96 kwa mwaka 2010 hadi kufikia wahandisi 379 kwa mwaka huu.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Mhandisi Patrick Balozi (kushoto) akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wahandisi Wanawake nchini Mhandisi Alice Isibike akielezea changamoto wanazokutana nazo wahandisi wanawake mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wahandisi wanawake nchini wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahandisi wanawake wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...