Na Agness Francis wa Globu ya Jamii
Jeshi la  Polisi Mkoa wa Temeke limewatia mbaroni wahalifu wa makundi ya ukabaji na uporaji  nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
Kwa mujibu wa kamanda wa mkoa huo Gilles Muroto watuhumiwa  wanaoshikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa  umri wao ni kati ya miaka 12-25,  na kwamba opresheni hiyo ilikamata watuhumiwa wa uhalifu 8 kutoka Mbande na wengine 8 kutoka Chamazi wilayani humo.
Hata hivyo wahalifu hao walikiri kuwa makundi na vishawishi ndio huwasababishia kufanya matukio hayo kwa kutumia visu na mapanga kwa kupora pochi za kina mama  kuchukua simu pamoja na fedha.
Kamanda Muroto pia  alikemea utoro wa wanafunzi   na kutaka wazazi kurejesha watoto wa mashuleni na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya msingi katika kupata elimu.
Nae mzazi Zuhura Hamza alisema watoto wenyewe ndio hawasikii na hawataki kusoma na kwamba wamejitahidi kadri ya uwezo wao lakini hawajapata suluhu la tatizo hilo hivyo akiomba msaada kwa wakuu wa shule.
Kamanda Muruto  alitoa wito kwa wazazi wawahimize watoto kwenda shule, kwani watoto wamezagaa mitaani na kujiingiza katika makundi mabovu  kama ya madawa ya kuevya, uporaji, uvuataji bangi na sigara.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Afande Gilles Muroto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwashikilia watuhumiwa wa makundi ya ukabaji na uporaji nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja na  wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akiwaonesha wanahabari watuhumiwa wa makosa mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...