Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) amesema Watumishi wa Umma walioghushi vyeti watachukuliwa hatua za
kinidhamu.
Mhe.
Kairuki alisema hayo katika kikao kazi na watumishi na viongozi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Temeke,Tarafa ya Mbagala mapema leo.
Mhe.
Kairuki alisisitiza kuwa wote walioghushi vyeti hawapo kazini na wameshafutwa katika
orodha ya malipo ya Serikali (payroll) na kuelekeza waajiri kuwafuta wote
wasiostahili kuwepo katika orodha ya malipo na wasimsubiri hadi afike katika
maeneo ya kazi ili kutekekeza hilo.
“Baada
ya zoezi la uhakiki kukamilika, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa
walioghushi vyeti kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo iliyopo
katika Utumishi wa Umma” Kairuki alisema.
Aidha,
aliwataka waajiri kuhakikisha wanahakiki taarifa za watumishi wapya wanapoajiriwa
na wale wanaohamia ili kujiridhisha kama wana vyeti safi.
“Ni wajibu
wa kila Mwajiri kuhakikisha kuwa Vyeti vya kila mwajiriwa mpya vinathibitishwa
na Mamlaka husika kabla ya kumwajiri na hatimaye kumuingiza kwenye Orodha za
Malipo ya Mishahara (Payroll) kupitia kwenye Mfumo wa HCMIS na Mifumo mingine
ya mishahara ya kitaasisi.”
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J.
Kairuki akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa tarafa ya Mbagala
Wilaya ya Temeke alipofanya ziara katika tarafa hiyo kwa ajili ya kusikiliza
kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Tawala
Wilaya ya Temeke Bw. Hashim Komba
Afisa
Elimu Kata ya Mbagala Kuu Bibi. Mindi Kuchilingulo akichangia mada wakati wa
ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe.
Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya
Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Tawala Wilaya ya Temeke Bw. Hashim Komba akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J.
Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala
Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhe. Waziri Angellah Kairuki
Mkurugenzi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma
Bw. Issa Ng’imba akielezea shughuli zinazofanywa na idara yake wakati wa ziara
ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah
J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala
Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya watumishi wa umma kutoka tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke wakifuatilia
hoja zilizokua zikiendelea wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za
watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es
Salaam. Picha na Genofeva Matemu - Maelezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...