Na Karama Kenyunko, Globu  ya jamii
Watu wawili, Safina Kassim Rupia na David Faustine Chimomo, wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.7 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa, kuwa, kati ya Julai 11 na Oktoba 28,2015 washtakiwa hao wakiwa Azam ICD Sokota walitenda makosa hayo.
Imedaiwa, siku hiyo washtakiwa walisababisha hasara ya Sh 12,618,970,229 kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipiwa kodi.
Katuga ameendelea kudai kuwa,siku hiyo katika bandari Kavu ya Azam ICD iliyopo Sokota katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walisaidia kukwepa kodi ya makontena 329 ambayo kodi yake ilikuwa na thamani ya sh. 12,618,970,229.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi ya uhujumu uchumi hadi Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa wakili Katuga, Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi 27,2017 itakapokuja kwa kutajwa.

Mtuhumiwa David Faustine Chimomo akiwa anatoka  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka ua uhujumu uchumi  na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.6 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha.


Mtuhumiwa Safina Kassim Rupia akiwa anatoka  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka ua uhujumu uchumi  na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.6 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...