Mtoto Lameck Charles (9) pamoja na mdogo wake Fredrick Charles (8) ni wanafunzi  wa shule ya Msingi Inteki wakiwa wanaonyesha mchezo wa sarakasi ndani ya stendi ndogo ya jijini Arusha  ikiwa ni sehemu ya kazi ambayo wanaifanya kipindi wakiwa likizo. 
Watoto hawa ambao  walikutwa na kamera yetu walisema kuwa wamekuwa wakitumia kipaji hicho walichojifunza kutoka kwa kaka yao kujipatia fedha ya kununulia vitu vidogo vidogo pindi pale wanaporejea shuleni.
Pembeni ni baadhi ya wananchi wakiwa wanawashuhudia watoto hao wakiendelea kuonyesha vipaji vyao. Wengi walipohojiwa walisema iko haja kwa wazazikutambua na kuendeleza vipaji vya watoto wao badala ya kuwaachia wanahangaika wenyewe. 
Picha na Woinde Shizza, Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...