THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAZIRI DKT. MAHIGA AKUTANA NA MCHUNGAJI ONGERE NA BALOZI WA IRAN NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Mchungaji John Oscar Ongere ambaye alifika ofisini kwa Mhe. Waziri kujadili maandalizi ya Kongamano kubwa la uwekezaji linalotarajiwa kufanyika nchini mwezi Novemba 2017. Kongamano hilo litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam litajumuiya wafanyabiashara wakubwa kutoka kote duniani na wa hapa nchini kujadiliana namna bora ya kutumia fursa lukuki za uwekezaji zilizopo hapa nchini.

Mchungaji Ongere akifanya maombi kwa ajili ya kuiombea nchi amani na utulivu ili iweze kukua kiuchumi
Picha ya pamoja
 Balozi wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Mousa Farhang ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili maandalizi ya sherehe za kumuapisha Rais Mteule wa Iran, Mhe. Hassan Rouhani zitakazofanyika Tehran tarehe 05 August 2017.

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo, Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bi. Zainab Angovi-Mrutu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw Ayoub Mndeme na Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu.

Ujumbe aliofuatana nao Balozi wa Iran ukifuatilia mazungumzo.